Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Ruzuku kwa ajili ya haki za Wanawake wenye Ulemavu: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara. 

Pata majibu kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Ruzuku kwa ajili ya haki za Wanawake wenye Ulemavu hapa chini. 

Kikundi chetu hakijasajiliwa – je tunaweza kutuma maombi? 

Ikiwa unaomba ruzuku ndogo (hadi $ 10,000) si lazima uwe umesajiliwa. 

Ikiwa unaomba ruzuku kubwa (hadi $20,000) basi unahitaji uwe umesajiliwa na mamlaka za serikali katika nchi yako. Ushirika au uanachama nje ya nchi hautakubaliwa, lakini unakaribishwa kutuma maombi ya ruzuku ndogo. 

Unamaanisha nini unaposema “kusajiliwa”? 

Ikiwa unaomba ruzuku kubwa (hadi $20,000) basi unahitaji kusajiliwa  na mamlaka za serekali katika nchi yako. Aina nyingine za usajili haziwezi kukubalika kwa kusudi hili. Ushirika au uanachama nje ya nchi hautakubaliwa. Tafadhali zingatia sio lazima uwe umesajiliwa kwa maombi ya ruzuku ndogo.  

Je, ni aina gani ya marejeleo au taarifa tunazohitaji kutoa, ikiwa sisi ni kikundi ambacho hakijasajiliwa? 

Makundi ambayo hayajasajiliwa yataulizwa kutoa majina na maelezo ya mawasiliano ya wadhamini wawili katika fomu ya maombi. Udhamini unaweza kutolewa na mtu yeyote anayekufahamu ambaye si mwanafamilia. Iwapo wadhamini utakaoandika wakati wa kutuma maombi si watu wa kitaaluma au watu wanaofahamika katika jamii, tunaweza kukuuliza hivi baadaye iwapo ombi lako litaendelea hatua zinazofuata. 

Ni aina gani ya ulemavu inatumika/kukubalika? 

Ikiwa kikundi chako kitajitambulisha kama kikundi cha watu wenye ulemavu, basi tutakubali ombi lako. 

Kwa nini ruzuku hii inalenga wanawake pekee? Wanaume pia ni sehemu ya harakati za watu wenye ulemavu. 

Katika mashauriano yetu na wanaharakati wa masuala ya watu wenye ulemavu, mara nyingi tunasikia kwamba wanawake wenye ulemavu wametengwa zaidi katika udhibiti wa fedha kuliko wanaume wenye ulemavu. Hii inasababisha ukosefu wa kuzingatia vipaumbele vyao na usaidizi mdogo katika kuchukua hatua na uongozi. Kwa hiyo ruzuku hii inalenga hasa wanawake. 

Hata hivyo, maandiko miradi ya ruzuku kutoka kwa mfuko huu yanaweza kuhusisha kazi zinazojumuisha wanaume, mradi tu kikundi kinachoomba kiongozwe na angalau 50% ya wanawake wenye ulemavu. 

ADD inaendelea kuchangisha fedha kwa ajili ya utoaji zaidi wa ruzuku kwa makundi mbalimbali yanayolengwa. 

Ni lazima kikundi kiwe na ukubwa gani ili kutuma maombi? 

Kikundi chako lazima kiwe na angalau wanachama watatu. 

Kwa nini haya ndio makundi ya kipaumbele? 

ADD imejitolea kusaidia makundi yaliyotengwa zaidi ndani ya vuguvugu la haki za watu wenye walemavu kupitia utoaji shirikishi wa ruzuku. Wanawake wenye ulemavu kutoka nchi za Ghana, Tanzania na Uganda waliobuni ruzuku hii wamebainisha makundi hayo kuwa ndiyo yaliyotengwa zaidi ambayo wangependa ruzuku hii kuyapa kipaumbele: 

Walitambua makundi haya kulingana na uzoefu wao wa kuishi na mazungumzo na kujifunza wao kwa wao.  

Unaweza kusoma zaidi kuhusu namna ADD imejitolea kusaidia makundi yaliyotengwa zaidi ndani ya vuguvugu la haki za watu wenye walemavu katika mpango mkakati wetu, Mtiririko: add.org.uk/mtiririko

Je, tunaweza kuwasilisha maombi ikiwa hatuna makao au kusajiliwa katika mojawapo ya nchi hizo tatu? 

Hapana, unahitaji kuwa katika nchi mojawapo ya hizi (Ghana, Tanzania, au Uganda). Shughuli zote za mradi lazima zifanyike katika moja au zaidi ya nchi tatu zilizotajwa. Tafadhali kumbuka kuwa ruzuku itatoa kipaumbele kwa mipango na shughuli zinazoongozwa ndani ya nchi. 

Je, ni lazima tuwe raia wa nchi hizo tatu? 

Hapana, hauhitaji kuwa raia wa nchi hizo. Tunataka ruzuku hiyo iwafikie watu wanaoishi katika mojawapo ya nchi hizo ambao huenda hawana uraia, kwa mfano, wakimbizi. 

Nchi yangu tayari imeridhia Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika kwa hiyo tufanye nini? 

Shughuli katika andiko lako zinaweza kusaidia kutetea utekelezaji wa Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika na kubadilishana ujuzi kuihusu, au shughuli nyingine zozote unazofikiri zitasaidia kuimarisha. Hii ni pamoja na kujenga harakati za wanawake wenye ulemavu ili kukuza usaidizi wa utekelezaji wa Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika na vifungu vyake. 

Kwa mifano zaidi tafadhali tazama ukurasa huu kwenye Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika.  

Je, ni shughuli gani zinazotizamiwa katika maandiko ? 

Shughuli nyingi utakazofanya zinafaa kuunga mkono uidhinishaji au utekelezaji wa Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika. Hii inaweza kuwa kutetea katika serikali za mitaa au kitaifa, kubadilishana taarifa kuhusu itifaki, au kubainisha mapungufu ya sasa katika utekelezaji wa itifaki. Hii inaweza pia kujumuisha kujenga mashirika na harakati zao ili kuendelea kufanya utetezi wenye nguvu zaidi kuhusu Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika. 

Ruzuku hii pia inalenga kuimarisha harakati za wanawake wenye ulemavu, hii inaweza kuwa kuimarisha au kusaidia shirika lako mwenyewe kukua au kuwa na nguvu kwa njia yoyote ambayo unadhani inahitajika zaidi, na kuunganisha na mashirika mengine na harakati. 

Tafadhali angalia orodha iliyo hapa chini ya maeneo ya vipaumbele kwa shughuli ambazo wanawake wa timu ya ubunifu wametoa: 

  1. Kujenga maendeleo ya shirika na uendelevu wa kifedha wa shirika au harakati zake.  
  2. Kujenga uelewa na kufanya utetezi juu ya Itifaki ya Masuala ya Ulemavu Afrika (African Disability Protocol) na sera nyingine zinazounga mkono.   
  3. Kujenga ujuzi juu ya utetezi.   
  4. Kusaidia uhamasishaji wa wanawake na wasichana wenye ulemavu kwa ajili ya kuchukua hatua.   
  5. Kuhimiza ushirikiano katika harakati za wanawake na wasichana wenye ulemavu, watu wengine wenye ulemavu na vyama vya watu wenye ulemavu, na harakati nyigine.   
  6. Kusaidia upatikanaji na ujumuishwaji wa makundi yaliyotengwa zaidi katika mbinu hizi.  

Je, kuna kiwango cha chini cha pesa unachoweza kuomba? Je, kuna kiwango cha juu unachoweza kuomba? Kuna tofauti gani kati ya ruzuku ndogo na ruzuku kubwa? 

Hakuna kiasi cha chini unachoweza kuomba. 

Ikiwa ungependa kutuma maombi ya $10,000 au chini ya hapo, basi utume maombi ya Ruzuku Ndogo. Hizi ziko wazi kwa vikundi, mashirika na harakati ambazo hazijasajiliwa na zilizosajiliwa. 

Ikiwa ungependa kutuma maombi kati ya $10,001 na $20,000 unaweza kutuma maombi ya Ruzuku Kubwa lakini tafadhali kumbuka kuwa hizi zinatumika tu kwa vikundi na mashirika yaliyosajiliwa na serikali ya kitaifa au ya mtaa katika nchi yako, na ambayo yamekuwa yakifanya kazi kwa angalau miaka 2. 

Kando na hitaji la usajili na uzoefu wa miaka miwili wa uendeshaji wa Ruzuku Kubwa, hakuna tofauti nyingine katika jinsi unavyoweza kupanga kutumia pesa kati ya Ruzuku Ndogo na Kubwa. 

Je, kuna muongozo wowote wa kuwasilisha bajeti ya mradi wangu? 

Mkakati wetu ni kutoa ufadhili ambao unaweza kunyumbulika iwezekanavyo. Unaweza kuona kwamba fomu ya maombi ni rahisi na wazi zaidi kuliko fomu nyingine. Hii ni kwa sababu ni juu yako unachotaka kufanya na ufadhili. Hakuna mahitaji yaliyowekwa kulingana na kiasi kinachoruhusiwa kwa vitu kama vile “gharama za shughuli” na “gharama za uendeshaji”. Tunaamini kwamba unajua vizuri zaidi jinsi unavyohitaji kutumia pesa, kwa hivyo tafadhali tuambie unachohitaji ufadhili, ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji na uendeshaji wa shirika. Tunafanya hivi makusudi ili kurahisisha utumaji maombi, na kuweka mchakato wazi na rahisi zaidi. 

Je kuna taratibu au mahitaji gani wakati wa uthibitishaji? 

Hii itategemea ukubwa wa kikundi au shirika linaloomba. Ikiwa maombi yako yatapitishwa kwenye hatua nyingine, kutakuwa na mazungumzo ya mwanzo ili kujadili masuala ya kifedha, ulinzi na utawala. 

Je, ninaweza kutuma maombi yangu katika fedha/sarafu gani? Je, ninaweza kutuma kwa fedha za Kitanzania au kwa US $? 

Unaweza kutuma maombi yako kwa sarafu ya nchi yako (shilingi ya Tanzania au shilingi ya Uganda au Ghana Cedi) au USD. 

Je, ikiwa maombi yetu yatafanikiwa, je, pesa zitapokelewa kwa USD au sarafu ya ndani? 

Fedha zitatolewa kwa sarafu au fedha ya nchi husika kulingana na kiwango cha kubadilisha fedha cha siku ambayo Makubaliano ya ushirikiano huu yatasainiwa. 

Je, tunaweza kuomba kama muungano wa kikundi au taasisi zaidi ya moja? Je, fedha za waombaji walioungana zitatolewa vipi? 

Unaweza kujiunga na mashirika au vikundi vingine kuwasilisha maombi yako pamoja ukipenda. Itakuwa juu yako kuamua jinsi fedha zitakavyogawanywa. ADD itafanya kazi nawe ili kubaini ni njia ipi itafanya kazi vyema zaidi kwa usimamizi wa fedha wa ruzuku yako. 

Mashirika ya wakimbizi yanaweza kuomba? 

Ndiyo, mashirika ya wakimbizi yanakaribishwa kutuma maombi, tafadhali rejelea ukurasa mkuu wa ruzuku ili kuona fedha tofauti zinazopatikana. 

Je shirika/vyama vya wazazi wa watoto wenye ulemavu (haswa wa akili au wale walio na ulemavu wa mfumo wa fahamu) wanaweza kuomba? 

Ruzuku hii ni kwa vikundi na mashirika ambayo yanaongozwa na wanawake wenye ulemavu (hii ina maana angalau nusu ya viongozi wa vikundi lazima wawe wanawake wenye ulemavu na ikiwa kuna bodi lazima iwe na angalau 50% ya wanawake wenye ulemavu) . 

Je, ninawezaje kujua zaidi kuhusu Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika?

Tafadhali tembelea ukurasa huu ili kujua zaidi add.org.uk/ADP-Swahili  

Je! ni idadi gani ya ruzuku mtakayotoa? 

Hatujui ni ruzuku ngapi tutatoa. Tuna ‘mfuko’ wa kuanzia wa fedha ambayo itagawanywa kati ya maombi yaliyofanikiwa, kulingana na kiasi wanachoomba. Kwa sasa tuna $66.7K katika kila ‘mfuko’ wa nchi kwa Ghana, Tanzania na Uganda. Tunaweza kuongeza ‘mfuko’ wa fedha ikiwa tunaweza kukusanya fedha zaidi. 

Je, tunaweza kutuma ombi ikiwa hatuna akaunti ya benki? 

Ndiyo. Ikiwa maombi yako yatafanikiwa, tutafanya kazi nawe kukubaliana njia bora zaidi kama sehemu ya kuanzisha ushirikiano, kwa mfano, kwa kutafuta mfadhili wa kifedha ili kupokea fedha kupitia yeye. 

Uendelevu – ni kwa kiasi gani ruzuku hii ni endelevu, kutakuwa na raundi za baadaye za ufadhili? 

Kwa sasa tunaangazia kutoa ruzuku hii na hakuna awamu ya baadaye iliyopangwa tayari. Hata hivyo, hii ni ruzuku ya majaribio kama sehemu ya mabadiliko yetu kama shirika na tunapanga kufanya utoaji ruzuku shirikishi zaidi na kuwa na fursa za siku zijazo za kutuma maombi ya ufadhili kutoka kwa ADD. 

Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu kazi za ADD International na fursa zozote zijazo za ruzuku shirikishi kwa kujiandikisha kwenye jarida letu hapa chini, au kutufuata kwenye Facebook, Instagram, Twitter (X) au LinkedIn.