Ruzuku kwa ajili ya haki za Wanawake wenye Ulemavu

Tunatambulisha Ruzuku yetu mpya na shirikishi.

Ruzuku kwa ajili ya haki za Wanawake wenye Ulemavu ni mfuko unaolenga mashirika ya ndani ya nchini Ghana, Tanzania na Uganda yanayosaidia Itifaki ya masuala ya Ulemavu ya Afrika (African Disability Protocol) na kuimarisha harakati za wanawake wenye ulemavu. Ruzuku hii imefanyiwa ubunifu na timu ya wanaharakati wanawake wenye ulemavu kutoka nchi hizo. 

Sasa maombi ya Ruzuku hii yamefungwa.


 Itifaki ya Masuala ya Ulemavu Afrika (African Disability Protocol) ni nini? 

 Itifaki ya Masuala ya Ulemavu Afrika (African Disability Protocol) ni mkataba wa kwanza wa haki za binadamu unaoshughulikia ubaguzi unaowakabili watu wenye ulemavu katika nchi za Afrika. Itifaki hii ni zaidi ya sheria zilizopo za haki za binadamu za Kiafrika, hasa kwa kushughulikia masuala kama vile mila, imani potofu na ushirikina unaodhuru watu wenye ulemavu. Kwa kutumia mbinu ya kijamii na haki za binadamu, inatambua uzoefu wa kipekee wa watu wenye ulemavu barani Afrika. 

Itifaki inahitaji kuidhinishwa ili kutekelezwa. Wazo ni kwamba ruzuku kutoka kwa mfuko huu zinaweza kutumika kuishawishi serikali kwa hili kutokea, na kusaidia utekelezaji baada ya kuridhiwa. 


Nani anaweza kutuma maombi?   

Ruzuku hii ni kwa ajili ya mashirika na vikundi vinavyoongozwa na wanawake wenye ulemavu nchini Ghana, Tanzania na Uganda kufadhili kazi zinazoimarisha na kusaidia wanawake wenye ulemavu waliotengwa zaidi katika nchi zao. 

Makundi haya ni pamoja na: Wanawake waliotengwa zaidi wenye ulemavu, wanawake wenye ulemavu katika maeneo ya vijijini, wasichana na wanawake vijana wenye ulemavu wenye umri kati ya miaka 12 – 35, wanawake wenye ulemavu wenye elimu duni, mashirika yenye wanachama katika ngazi ya chini/mashinani, wanawake wazee wenye ulemavu zaidi ya miaka 65. Makundi haya yaliyolengwa yalitambuliwa na wanawake wenye ulemavu waliobuni ruzuku hii. 

Shughuli au mipango inayopendekezwa lazima pia izingatie angalau mojawapo ya maeneo ya kipaumbele yaliyochaguliwa na wanawake waliobuni ruzuku hii. Hizi ni: 

  1. Kujenga maendeleo ya shirika na uendelevu wa kifedha wa shirika au harakati zake. 
  2. Kujenga uelewa na kufanya utetezi juu ya Itifaki ya Masuala ya Ulemavu Afrika (African Disability Protocol) na sera nyingine zinazounga mkono.  
  3. Kujenga ujuzi juu ya utetezi.  
  4. Kusaidia uhamasishaji wa wanawake na wasichana wenye ulemavu kwa ajili ya kuchukua hatua.  
  5. Kuhimiza ushirikiano katika harakati za wanawake na wasichana wenye ulemavu, watu wengine wenye ulemavu na vyama vya watu wenye ulemavu, na harakati nyigine.  
  6. Kusaidia upatikanaji na ujumuishwaji wa makundi yaliyotengwa zaidi katika mbinu hizi. 

Ni fedha kiasi gani zinaweza kuombwa 

Aina mbili za ruzuku zitatolewa:

Ili kuomba ruzuku kubwa kikundi lazima kiwe kimesajiliwa. 


Tarehe muhimu.

Maombi yatafungwa saa sita usiku, saa za Afrika Mashariki, siku ya Jumamosi tarehe 31 Agosti.

Ni lazima upange kutumia fedha/ruzuku yote ndani ya miezi 12.


Je, maamuzi ya ruzuku yatafanywaje?

Ruzuku hii imeundwa kwa pamoja na maamuzi yatafanywa kwa ushirikiano baina ya timu ya ADD International na wanawake wenye ulemavu.

Waombaji wote watapata mrejesho kutoka kwetu. Ikiwa hujasikia chochote kufikia tarehe 1 Oktoba tafadhali wasiliana na disabilityjusticewomen@add.org.uk. 


Usalama na Ulinzi.

Ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu usalama wako wakati wa mchakato wa kutuma maombi na ungependa kuzungumza nasi, tafadhali tutumie barua pepe kwa disabilityjusticewomen@add.org.uk au kwenye WhatsApp kupitia +254 735 486754

Malalamiko na Maoni

Ikiwa ungependa kuwasilisha malalamiko au kutoa baadhi ya maoni kwa ADD kuhusu mradi huu tafadhali wasiliana na Rose Tesha, Mkurugenzi wa Afrika, kwa barua pepe rose.tesha@add-tanzania.org au piga simu +255 22 2780336; +255784316556 au +255713316556. 

Ulinzi na usalama  

ADD inatarajia viwango vya juu vya maadili na taaluma kutoka kwa wafanyakazi na wawakilishi wetu wote. Kwa maelezo zaidi kuhusu ulinzi na usalama katika Shirika la ADD, au kueleza wasiwasi wako kuhusu tabia, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa tovuti wa ulinzi na usalama: add.org.uk/safeguarding