Mwaka 2025 ni mwaka maalum kwa shirika la ADD International, tukisherehekea kutimiza miaka 40.
Kwa miongo minne, tumekuwa tukifanya kazi kwa pamoja – jumuiya ya kimataifa ya wanaharakati wenye shauku na waliojitolea kutetea haki za watu wenye ulemavu – kuendelea kuhamasisha juu haki za watu wenye ulemavu na kuunda ulimwengu jumuishi zaidi.
Katika kusherehekea, tunataka kuthamini safari hii ya mafanikio makubwa ya vuguvugu la haki za watu wenyeulemavu kote ulimwenguni na sauti ambazo zimepazwa katika kuliunda.
Kuanzia kwa wanaharakati barani Asia na Afrika hadi wafuasi nchini Uingereza, hadithi na uzoefu wako ni muhimu katika kusimulia hadithi hii kwa pamoja.
Tunatamani kusikia kutoka kwako. Tuambie hadithi yako na kwa pamoja, tusherehekee mafanikio ambayo tumepata na iwe chachu ya kuhimiza zaidi haki za watu wenye ulemavu.
Jinsi inavyofanya kazi.
- Tushirikishe Hadithi Yako: Jibu maswali machache kuonyesha uhusiano wako na vuguvugu la utetezi wa haki za watu wenye ulemavu. Jibu tu maswali ambayo unahisi una utayari wa kuyajibu.
- Weka Picha: Weka picha inayoendana na hadithi yako, Picha hii inaweza kuwa yako, jumuiya yako, au picha inayoweza kuwa na maana fulani katika safari yako.
Idhini kwanza.
Tunaheshimu faragha yako na kabla ya kutushirikisha hadithi yako, tungependa usome fomu yetu ya idhini na uhakikishe kuwa umeridhia kutushirikisha hadithi na picha zako.
Soma fomu yetu ya idhini
ADD International hutoa machapisho mbalimbali ili kuwasaidia watu kuelewa kazi zetu na tunatoa machapisho haya katika hadhira mbali mbali na za kimataifa. Tunapenda kushirikisha uzoefu wa watu ambao tunafanya kazi nao katika mawasiliano yetu kwani inasaidia kuonyesha mabadiliko ambayo kazi yetu inaleta. Kwa kutupa idhini yako kushirikisha wengine hadithi yako, unatupa ruhusa ya kuitumia katika mawasiliano yetu kwa miaka 5 ijayo.
Usalama wako ndio kipaumbele chetu. Tafadhali zingatia kama kuna athari yoyote inayoweza kutokea kutokana na picha ama hadithi yako kuwekwa hadharani. Haulazimishwi kushiriki na ni haki yako kuamua kushiriki kama umeridhia kutushirikisha na unaona ni vema kufanya hivyo. Ikiwa utashiriki, unaweza kujiondoa wakati wowote. Ukiamua ama kuona kuwa kuna mazingira yanakunyima furaha kwa kuendelea kushirikisha hadithi yako unaweza kujiondoa wakati wowote kwa kuwasiliana na communications@add.org.uk
Hadithi yangu watashirikishwa nani? ADD International hushirikisha machapisho yake kwa wafuasi, mashirika mengine ya misaada, watoa huduma, na viongozi katika eneo lako, nchi na kimataifa. ADD International ina hadhira kubwa ya kimataifa na hatuwezi kudhibiti ni nani anayeona machapisho yetu. Tafadhali fikiria kuhusu kama kuna hatari zozote kwa usalama wako ikiwa hadhira fulani itajua hadithi yako. Maudhui tunayokusanya kutoka kwako yatahifadhiwa kwa usalama na wafanyakazi wa ADD International walioidhinishwa kuyafikia. Faili zote zitapewa namba maalum na kuhifadhiwa tofauti na majina yoyote au alama za utambulisho wa moja kwa moja. Hatutahifadhi taarifa zako kwa zaidi ya miaka 5.